Thursday, June 10, 2010

Benitez ahamia inter..........


baada ya kutemwa liverpool sasa atapa dau kwa inter ameshafanya mkataba wa miaka 2.

Friday, June 4, 2010

Liverpool Yamtema Benitez


Baada ya Liverpool kuvurunda msimu uliopita na kumaliza ligi ikiwa imeshika nafasi ya saba, kocha wa Liverpool Rafa Benitez amepoteza kazi yake baada ya miaka sita ya kuiongoza Liverpool.
Rafa Benitez ametemwa na Liverpool baada ya miaka sita kufuatia kufanya vibaya kwa Liverpool katika msimu uliopita.

Liverpool ilimaliza ligi ikishika nafasi ya saba, ilitolewa mapema kwenye makombe ya Carling na kombe la FA, haikufika kokote kwenye kombe la mabingwa wa ulaya kabla ya kutolewa nusu fainali kwenye kombe la UEFA.

Liverpool imemlazimisha Benitez achukue mikoba yake kwa kukatisha mkataba wake na kumlipa fidia ambayo inakadiriwa kufikia paundi milioni sita.

Benitez mwenye umri wa miaka 50 alisema baada ya kujulishwa kuwa kibarua chake kimeota mbawa: "Nina huzuni sana kutangaza kuwa sitaendelea kuwa kocha wa Liverpool FC. Napenda kuwashukuru wafanyakazi wote na wachezaji kwa juhudi zao".

Mwenyekiti wa Liverpool, Martin Broughton aliongeza: "Rafa ataendelea kukumbukwa na Liverpool kwa kutuletea kombe la mabingwa wa ulaya katika fainali dhidi ya AC Milan mjini Istanbul".

Broughton aliongeza kuwa baada ya msimu ambao haukuwa na matokeo mazuri, Liverpool imeona ni bora ijijenge tena upya.

Mchakato wa kutafuta kocha mpya wa Liverpool umeanza.

source nifahamishe