Sunday, April 3, 2011

Jambazi 'Obama' Atiwa Mbaroni



Polisi wa nchini Austria wamemtia mbaroni mwanaume mmoja wa nchini humo ambaye alikuwa akifanya matukio ya uporaji pesa kwenye mabenki akiwa amevaa kinyago chenye sura ya rais wa Marekani, Barack Obama.
Taarifa ya polisi wa Vienna, Austria imesema kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 45 raia wa Ujerumani anatuhumiwa kupora pesa kwenye benki zipatazo 7 za nchini humo ambapo wakati wote alikuwa akivaa kinyago chenye sura ya Barack Obama.

Polisi walisema kuwa tangu mwaka 2008, mwanaume huyo alifanya matukio 7 ya uporaji pesa kwenye mabenki na tukio lake la mwisho la uhalifu alilifanya mchana wa siku ya alhamisi katika kijiji cha Fornach.

Msako wa polisi ulianza na alitiwa mbaroni muda mfupi baadae baada ya mbwa wa polisi kufanikiwa kukiona kinyago na silaha alizokuwa akizitumia jambazi huyo.

Jambazi huyo alikiri kufanya matukio ya ujambazi na polisi walitangaza kuwa wana furaha wamemtia mbaroni jambazi waliyekuwa wakimtafuta kwa muda mrefu.


source nifahamishe