Tuesday, December 15, 2009

Kili Stars Yawasili Na Mfungaji Bora Wa Chalenji


BAADA ya kushindwa kutwaa ushindi wa tatu wa michuano ya Kombe la Chalenji, timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kili Stars’ inatarajiwa kuwasili nchini mchana huu ikitokea Kenya.
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela, alisema timu hiyo itawasili mchana huu katika Uwanbja wa ndege wa Julius Nyerere.

“Tunaomba wadau wajitokeze kuja kuipokea timu yetu ya taifa, lengo ni kuwapa hamasa wachezaji wetu kwa maendeleo ya zoka letu,” alisema Mwakalebela.

source.nifahamishe

Kili Stars inawasili na mfungaji bora wa Kombe la Chalenji Mrisho Ngassa aliyefunga mabao matano.

No comments:

Post a Comment