Monday, May 31, 2010
Eto'o Atishia Kuitosa Cameroon Baada ya Kukosolewa na Roger Milla
Nyota wa timu ya taifa ya Cameroon, Samuel Eto'o ametishia kujitoa kwenye timu ya Cameroon itakayoshiriki kombe la dunia baada ya kukosolewa na mkongwe wa soka Afrika, Roger Milla.
Mshambuliaji wa Inter Milan Samuel Eto'o ametishia kususia kuichezea Cameroon baada ya kukosolewa na nyota wa Cameroon wa kombe la dunia la 1990, Roger Milla kuwa hajitumi anapoichezea timu ya taifa.
Akiongea hivi karibuni na vyombo vya habari, Roger Milla alimkosoa Eto'o akisema kuwa Eto'o hujituma zaidi anapoichezea yake ya Inter Milan kuliko anapoichezea timu yake ya taifa.
Akiongea na televisheni ya Canal Plus Sport ya Ufaransa, Eto'o alielezea kukasirishwa na maoni ya Roger Milla na kuongeza kuwa huenda akajitoa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon kitakachoshiriki fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini.
"Kwani kombe la dunia ndio la muhimu sana kwangu?", alisema Eto'o.
"Bado nina siku chache za kufikiria nichukue uamuzi gani kwakuwa huwa sipendi mambo kama haya", aliongeza Eto'o.
"Roger Milla amefanya nini cha maana? amewahi kuchukua kombe la dunia? timu yake ya mwaka 1990 iliishia robo fainali", alisema Eto'o kwa hasira.
Hata hivyo pamoja na Eto'o kutishia kuitosa Cameroon, kocha wa Cameroon, Paul Le Guen alimtaja Eto'o kwenye kikosi chake cha wachezaji 23 kitakachoenda Afrika Kusini kwenye fainali za kombe la dunia.
Kikosi kamili cha Cameroon ni kama ifuatavyo:
Hamidou Souleymanou (Kayserispor), Carlos Kameni (Espanyol), Guy Roland Ndy Assembe (Valenciennes); Benoit Assou-Ekotto (Tottenham), Sebastien Bassong (Tottenham), Gaetan Bong (Valenciennes), Aurelien Chedjou (Lille), Geremi (Ankaragucu), Stephane Mbia (Marseille), Nicolas Nkoulou (Monaco), Rigobert Song (Trabzonspor); Eyong Enoh (Ajax), Jean II Makoun (Lyon), Georges Mandjeck (Kaiserslautern), Joel Matip (Schalke), , Landry Nguemo (Celtic), Alexandre Song (Arsenal); Vincent Aboubakar (Coton Sport), Eric Choupo-Moting (Nuremberg), Achille Emana (Betis), Samuel Eto'o (Inter Milan), Mohamadou Idrissou (Freiburg), Achille Webo (Mallorca).
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment