Monday, March 22, 2010

Manchester United Yaikong'oli Liverpool 2-1


Manchester United imerudi tena kileleni mwa ligi ya Uingereza baada ya kufuta uteja wake kwa Liverpool kwa kuipa kichapo cha mabao 2-1 kwenye uwanja wa Old Trafford jijini
VIDEO - Manchester United Yaikong'oli Liverpool 2-1


Wachezaji wa Manchester United wakipongezana Sunday, March 21, 2010 7:55 PM
Manchester United imerudi tena kileleni mwa ligi ya Uingereza baada ya kufuta uteja wake kwa Liverpool kwa kuipa kichapo cha mabao 2-1 kwenye uwanja wa Old Trafford jijini Manchester. VIDEO za magoli yote katika mechi hii mwisho wa habari hii.
Matumaini ya Liverpool kutwaa nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya Uingereza ili kuweza kucheza kombe la mabingwa wa ulaya msimu ujao yamezidi kufifia baada ya kupoteza pointi zingine muhimu kwa Manchester United.

Liverpool iliingia uwanjani ikiwa na nia ya kuiharibia Manchester United kampeni yake ya kutwaa ubingwa wa Uingereza kwa mara 19 na hivyo kuivuka rekodi ya Liverpool ya mataji 18.

Iliwachukua dakika tano tu Liverpool kuweza kupata goli la kuongoza kupitia kwa Fernando Torres ambaye aliunganisha vyema krosi ya Dirk Kuyt na kumwacha kipa wa Manchester United, Edwin van der Sar aking'ang'aa macho.

Manchester United ilipewa penalti dakika tano baadae baada ya Javier Mascherano kumuangusha Antonio Valencia kwenye mstari wa 18. Wayne Rooney alipiga penalti hiyo ambayo iliokolewa na kipa wa Liverpool, Pepe Reina lakini mpira ulipomrudia tena Rooney hakufanya ajizi kuuzamisha nyavuni.

Jahazi la Liverpool lilizama kwenye dakika ya 15 ya kipindi cha pili wakati Park Ji-sung alipopiga mbizi na kuunganisha kwa kichwa krosi ya Gary Neville.

Goli hilo lilidumu hadi wakati refa wa mechi hiyo alipopuliza kipyenga cha kumaliza mpambano huo
source nifahamishe

No comments:

Post a Comment