Friday, January 29, 2010

Chama cha riadha Zanzibar chataka kuandaa riadha taifa

CHAMA cha Riadha Zanzibar (ZAAA) kimeomba kuandaa mashindano ya Taifa ya mchezo huo kwa mwaka huu yanayotarajia kufanyika mwezi Mei.

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania, RT, Suleimani Nyambui alisema tayari wamepokea mwaliko kutoka ZAAA kuhusiana na maombi hayo.

Alisema maombi ya ZAAA yatajadiliwa katika kikao cha Kamati ya Ufundi ya RT kabla ya kutolewa uamuzi.

"ZAAA wametuletea barua hapa kuomba kuandaa mashindano ya Taifa bila shaka wameshawishika kufanya hivyo baada ya kuufanyia ukarabati Uwanja wa Amani hususani ile sehemu ya kukimbilia pamoja na ile saa ya kurekodi muda wa kukimbia," alisema Nyambui.

Mara ya mwisho Zanzibar iliandaa mashindano ya riadha ya Taifa mwaka 1971.


source mwananchi

No comments:

Post a Comment