Friday, January 29, 2010
Nahodha wa Uingereza Ajivinjari na Mpenzi wa Mchezaji Mwenzake
Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na timu ya Chelsea ya jijini London, John Terry ambaye ana mke na watoto wawili alijivinjari na mpenzi wa mchezaji mwenzake wa Chelsea na alipogundua siri imefichuka alikimbilia mahakamani kuchukua kibali cha kuwazuia waandishi wa habari kufichua siri hiyo.
John Terry nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na timu ya Chelsea, mume na baba wa watoto wawili, aliisaliti ndoa yake na kutembea na mpenzi wa mchezaji mwenzake Wayne Bridge aliyekuwa akiichezea Chelsea kabla ya kuhamia Manchester City.
John Terry aliposhtukia waandishi wa habari wamelinyaka soo hilo, alikimbilia mahakamani kuchukua kibali cha kuwazuia waandishi wa habari kuandika habari hiyo kwenye magazeti.
Kibali hicho kilitolewa kwa muda lakini leo pingamizi la mahakama liliondolewa na hivyo magazeti kuwa huru kumuandika John Terry alivyoisaliti ndoa yake na kumla uroda mpenzi wa rafiki yake.
Taarifa zinasema kwamba Terry alianza kujivinjari na mpenzi wa Wayne Bridge mrembo wa Ufaransa, Vanessa Perroncel, baada ya Wayne Bridge kuhama Chelsea na kuhamia Manchester City mwezi januari mwaka jana.
Vannessa ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume wa Wayne Bridge mwenye umri wa miaka mitatu, alibakia jijini London wakati Wayne Bridge alihamia mjini Manchester.
Wayne Bridge na Vannesa waliachana mwezi uliopita.
Hili ni skendo la pili kumkumba John Terry, mwaka 2003 alitiwa mbaroni kwa kupigana kwenye ukumbi wa starehe lakini baadae aliachiwa huru.
Wazazi wake nao ni maarufu magazetini kwa maskendo yaliyozua maswali mengi na kumtia aibu milionea John Terry.
Wakati mama yake alikamatwa akiiba nguo kwenye supermarket, baba yake alinaswa akiuza madawa ya kulevya.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment