Thursday, March 25, 2010

Messi Amuovateki Beckham Kwa Kuchukua Mshiko Mkubwa


David Beckham sio tena mcheza soka anayelipwa pesa nyingi kuliko wote kwani hivi sasa nyota wa Barcelona, Lionel Messi ndiye yupo kwenye chati anaingiza mshiko mkubwa zaidi kwa mwaka kuliko wachezaji wote duniani.
Lionel Messi nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina ndiye mchezaji anayekamata mshiko mkubwa zaidi kwa mwaka kuliko wachezaji wote duniani.

Kwa mwaka, Messi anajiingizia kiasi paundi milioni 29.6 ambazo ni milioni 2.3 zaidi ya anazoingiza David Beckham.

Kwa mwaka Messi anapokea mshahara wa paundi milioni 9, analipwa bonasi ya paundi milioni 3.6 na anaingiza paundi milioni 17.1 kutokana na matangazo ya makamapuni mbali mbali kama vile adidas, Pepsi na Gillette.

Katika listi ya wachezaji 10 wanaojiingizia kipato kikubwa kwa mwaka, nyota wa Cameroon, Samuel Et'oo anashika nafasi ya 10 kwa kiasi chake cha paundi milioni 12.4.

Hata hivyo wachezaji wa soka bado hawajafanikiwa kuwaovateki kwa kipato wachezaji wa mpira wa kikapu na gofu.

Tiger Woods ndiye mwanamichezo anayeingiza mshiko mkubwa kuliko wanamichezo wote duniani, anayemfuatia ni mchezaji mwenzake wa gofu Phil Mickelson huku nyota wa mpira wa kikapu, LeBron James akishika nafasi ya tatu.

Orodha kamili ya wanasoka 10 wenye kipato kikubwa kwa mwaka ni kama ifuatavyo:
1. Lionel Messi (Barcelona) £29.6m

2. David Beckham (LA Galaxy) £27.3m

3. Cristiano Ronaldo (Real Madrid) £26.9m

4. Kaka (Real Madrid) £16.9m

5. Thierry Henry (Barcelona) £16.2m

6. Ronaldinho (AC Milan) £15.4m

7. Carlos Tevez (Manchester City) £13.8m

8. Zlatan Ibrahimovic (Barcelona) £13m

9. Frank Lampard (Chelsea) £12.7m

10. Samuel Eto’o (Inter Milan) £12.4m


source nifahamishe

No comments:

Post a Comment